Nchi ya Tanzania imejipata katika orodha ya mataifa zinazotumia ukatizaji wa mtandao kama silaha dhidi ya wananchi wao wakati wa uchaguzi. Katika wakati uliojiri kabla uchaguzi wa kirais Oktoba 28 2020, mashirika yanayohusika na mawasiliano yalichukua hatua mbalimbali kukatiza haki za kidijitali za wananchi wa Tanzania. Shirika la Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA), haswa kwa maagizo ya uongozi wa Magufuli liliamrisha mashirika yanayotoa huduma za kusambaza intaneti na mawasiliano kuweka vifaa vya kuchuja mawasiliano katika mtandao kutoka shirika la kiisraeli, Allot, na kisha kasababisha msuosuo wa mitandao ya kijamii Twitter, WhatsApp na Telegram siku moja kabla ya uchaguzi.
Shirika la TCRA awali liliamrisha watoa huduma za mtandao kukatiza matumizi ya jumbe fupifupi na mawasiliano ya kisauti, Watanzania wakibaki bila njia murua za kuwasilana. Kwa sasa, mashirika haya bado yamezuia mtandao wa kijamii wa Twitter na wananchi hawajaweza kuutumia mtandao huo bila kutumia VPN, ambazo pia uongozi umepiga marufuku.
Hatua hizi zinadhuru haki za kibinadamu za WaTanzania, zikiwemo uwezo wa kuafikia habari na Uhuru wa kujieleza. Kutumia Shutdown Stories project, Access Now imenakili ripoti mbalimbali utakavyoona ili kuonyesha jinsi ambavyo kuzimwa kwa mtandao kunaadhiri maisha ya wananchi kikazi, kimasomo, kibiashara na katika mahusiano. Imeonekana wazi kwamba kuzimwa kwa mtandao kunaadhiri pakubwa maisha ya wananchi. Uongozi wa Tanzania umekatiza uwezekano wa wananchi kuafikia habari mbalimbali na wa kuhusika kwa uchaguzi, pamoja na kuadhiri maisha ya wananchi ya kila siku na operesheni za kibiashara.
Tupa jicho sasa kwa baadhi ya habari zinazoonyesha jinsi ambayo kuzimwa kwa mtandao unaadhiri maisha ya wananchi wa Tanzania. Kunazo njia pia ambazo wewe msomaji unaweza kuangazia madhara haya kwa niaba ya walioadhirika.
Raul Gil ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na pia ni mwandishi wa habari. Anatumia mtandao kawaida kwa kutekeleza kazi zake za kishule na kupata dondoo mbalimbali za habari.Raul vilevile ni mbunifu wa vitu vya urembo na hutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yake. Shughuli hizi zote ziliadhirika mtandao ulipozimwa.
Kama mwalimu na influencer, Godfrey Abely Magehema alijipata katengwa kutokana na taarifa chungu nzima wakati wa uchaguzi kwa vile mtandao ulizimwa.
Zainabu Makombe ni mkurugenzi wa shirika linalojishughulisha na haki za watoto. Kuzimwa kwa mtandao kuliadhiri pakubwa shughuli za shirika hilo.
Kibiriti Ngoma ni mwanasheria na mjasirimali na hutumia mtandao kama njia mojawapo kupata biashara na wateja. Mtandao ulipozimwa, Kibiriti na wateja wake iliwabidi kutumia VPN ambazo watu wengi hawana uzoefu wa kuzitumia na pia wakati mwigine inalazimu kuzilipia.
Kigogo alitatizika sana na shida zilizokumba mawasiliano kutokana na amri zilizotolewa na serikali ambazo ziliadhiri mtandao pamoja na SMS.
Idd Ninga anafanya kazi za jamii Arusha, Tanzania. Kuzimwa kwa mtandao kuliadhiri uwezo wake na haki yake kupata habari mbalimbali katikati ya wakati muhimu wa uchaguzi. Alishangaa sana kuwa wananchi hawakupata taarifa kabla ya mtandao kuzimwa.
Zaituni Njovu,anayefanya kazi za jamii aliadhirika kisaikolojia kwa vile kuzimwa kwa mtandao kuliadhiri kila kipengele cha maisha yake
Katika kazi zake kama Community Coordinator Dodoma, Tanzania, Maria kawaida hutumia simu na tarakilishi kuendeleza kazi zake. Mtandao ulipozimwa alishindwa kuendeleza kazi zake.
Kuzimwa kwa mtandao kulimsikitisha Florah Amon, mwanahabari ambaye kazi yake hutegemea mtandao.
Christina Gauluhanga ni mwandishi Tanzania. Uzimaji wa mtandao uliwaadhiri kikazi yeye na waandishi wenzake.
Kidawa Mwakaseko ni mwanaharakati wa maswala ya usalama mtandaoni. Aliwafunza jamaa na marafiki wake kutumia VPN.
Unavyoweza kusaidia
Mwaka wa 2020 pekee uongozi wa Togo, Burundi, Guinea, Belarus na Myanmar umesababisha msuosuo wa mtandao na mawasiliano wakati wa uchaguzi. Hatua hizi zinaathiri haki za wananchi husika za kujieleza, kuafikia habari na za kuhusika katika uchaguzi- unaweza kusaidia kukomesha matukio ya aina hii.
Saidia kuupa sauti ushauri wa #KeepItOn coalition kwa uongozi mbalimbali duniani kusitisha matumizi ya uzimaji wa mtandao kukiuka haki za wananchi vifuatavyo;
Sambaza makala haya katika mitandao ya kijamii kutumia hashtag #KeepItOn na #InternetShutdown kuangazia madhara ya kuzimwa kwa mtandao kwa maisha ya wananchi husika. Unaweza pia kuretweet @AccessNow hapa.
Sambaza fomu ya hadithi za kuzimwa kwa mtandao kwa jamaa na marafiki zako ili kutusaidia kupata ushuhuda zaidi; ili kuendeleza harakati zetu; ambazo zaweza kutumika kama ushahidi wa madhara kortini na barazani mbalimbali kimataifa.
Jielimishe
#KeepItOn ni kampeni ya kimataifa inayohusisha zaidi ya mashirika 220 duniani ambayo yameungana kupiga vita uzimaji wa mtandao kupitia maelimisho, msaada wa kiteknolojia, msaada wakisheria na kadhalika.
Iwapo una maswali zaidi yanayohusu kuzimwa kwa mtandao, sikiliza podcast yetu wa KillSwitch.